UWT MKOA WA MJINI UNGUJA IMEFANYA DUA MAALUM YA KUWAOMBEA VIONGOZI WA NCHI NA TAIFA


JUMUIYA ya Wanawake Umoja wa Wanawake(UWT),mkoa wa Mjini visiwani hapa jana imefanya dua maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika ofisi ya mkoawa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Dua hiyo ilianza kufanyika saa mbili asubuhi huku viongozi mbalimbali wa UWT akiwemo Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mjini Halima Sheha Mbwala, Katibu wa Baraza la Wazee la CCM Zanzibar,

Khadija Jabil,Mwakilishi wa Viti Maalum mkoa wa Mjini Sada Mwenda,muasisi wa jumuiya ya wanawake wa Afroshiraz Party(ASP) Sihaba Ismail Farhan walihudhuria kwenye dua hiyo.

Akizungumza mara baada ya dua hiyo Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Mjini Halima Sheha Mbwala alisema  jumuiya hiyo imeamua kufanya dua hiyo kumuombea Rais Samia pamoja na viongozi wengine ambao  wanaendelea kuchaguliwa kwa awamu hii.

"Tuna muombea mwanamke mwenzetu Rais Samia dua  kutokana na kuwa yeye ni mama kama sisi pia tumempa kipaumbele sana cha kumuombea dua hii na nchi yetu iwe salama na yeye amtulie nguvu zaidi," alisema 

Alisema katika dua hiyo jumuiya hiyo imeamuombea pia Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi ili washikamane na Rais Samia ili nchi yetu ifikie mahala ambapo Hayati Dk.John Magufuli alipaacha.




Mwenyekiti huyo alisema kutokana na kuwa Rais  Samia kwa sasa ndiye ameshika nafasi hiyo na  alikuwa mwenza wake jumuiya hiyo inaamini atafanikiwa vyema.

Kwa upande wake Katibu wa UWT mkoa wa Mjini Stamili Omary Bendego alisema lengo la dua hiyo ni kumuombea Rais Samia Mungu ampe nguvu katika  kipindi hiki cha uongozi wake.

"Tuna muombea kwa Mungu amuondolee husda ili atuongoze sisi watanzania pia tunamuombea Rais Dk.Mwinyi ampe hekima nguvu aweze kuwaongoza  wanzanzibar na hii ndio lengo la dua hii,"alisema

Alisema UWT imeamua kufanya dua hiyo kama viongozi hao wanavyowaomba wananchi kuwaombea na ndio uongozi wa jumuiya hiyo imeamua kufanya hivyo.   

Alisema wamefanya dua kummshukuru Mwenyezi Mungu na kumuomba amjalie kheri na baraka Rais Samia pamoja na hekima kwenye uongozi wake kutokana na kuwa yeye ndiye aliyemuweka katika nafasi hiyo.

"Pia tumeomba Mungu atujalie hali ya amani kwa lengo la watanzania tusikilizane ili waletewe maendeleo ambao wananchi wanayataka,"alisema

Alisema UWT inatarajia makubwa kwa Rais Samia na kwamba  atayaendeleza yale mambo makubwa aliyoyafanya hayati Rais  Dk.John Magufuli kutokana na kuwa yeye binafsi amekuwa akizungumza kuwa atayaendeleza hayo yote mazuri yalioanzishwa na serikali ya awamu ya tano.

No comments:

Post a Comment