MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo April 25,2021 ameongoza Kikao Maalumu cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.
Kikao hicho cha siku moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimepokea na kujadili mapendekezo ya wana CCM wanaomba kujaza nafasi wazi za uongozi katika Chama ambapo mapendekezo ya Wana CCM wanaoomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Mji Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kikao hicho pia kimepokea na kujadili mapendekezo ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge wanaoomba kuteuliwa kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kikao hicho ni maalumu kilichojadili masuala mbali mbali ya Chama kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977 Toleo jipya la 2017.
Kwa upande wa wajumbe wa Kikao hicho wamempongeza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa juhudi zake za kuongoza Chama kwa ueledi na juhudi kubwa hali inayosababisha Chama kupata mafanikio makubwa ya kisiasa yakiwemo upatikanaji wa ushindi katika uchaguzi mkuu wa dola pamoja na chaguzi ndogo.
“Umekuwa kiongozi wetu kwa muda mrefu tunajivunia kufanya kazi na wewe kwani kila siku tunajifunza mambo mengi mazuri ya kiutendaji na kiuongozi yanayotusaidia katika maeneo yetu ya kiutendaji”, walisema wajumbe wa mkutano huo.
Mapema mara baada ya kuanza kikao hicho Dk. Shein, aliongoza wajumbe hao kumuombea dua aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk. Abdulla JumaMabodi, akizungumza katika Kikao Maalum cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, kilichofanyika katika Ofisi za Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
No comments:
Post a Comment