Kikao cha Wawakilishi wa Chama Cha Mapinduzi kupitia Baraza la Wawakilishi, Kimefanya uchaguzi wa kuwachagua Wawakili watatu kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na pia Mkamu wa Rias wa Pili wa Zanzibar MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA akitumbukiza karatasi ya kupigia kura katika sanduku la kura,
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI ZANZIBAR amnacho kimeongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA, kimewachaguwa NDG. JAMAL KASSIM ALI, ND. MASOUD ALI MOHAMMED NA RIZIKI PEMBE JUMA Kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Pia amewataka Wajumbe Waliochanguliwa kiwakilisha vyema kupitia misingi ya CHAMA CHA MAPINDUZI kufuatia Katiba, Sheria, Kanuni, Miongozo na maelekezo ya CHAMA CHA MAPINDUZI. kufanya hivyo kutawajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa na kukiongezea sifa CHAMA CHA MAPINDUZI kwa kusimamia demokrasia na uongozi bora.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadall (mabodi) akiwa katika kikao cha uchaguzi wa nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
No comments:
Post a Comment