MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Mwantumu Mdau Haji akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa kusini ambao wamejiunga na kikoba katika ukumbi wa Afisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya kusini Unguja.
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa kusini Unguja Mhe. Mwamtumu Mdau Haji, amezindua kikundi cha wanawake Vicoba Wilaya ya Kusini, amesema kuwa Vicomba vimetokea Bungeni na mpaka kufika kwao kwaiyo wanatakiwa kuvizingatia na kuendeleza mshikamano wao ili kujikwamua kiuchumi na kufanikisha malengo yao kwa kuendeleza mshikamano.
Napia katika muamko wao wa kikundi ichi aliwachangia shilingi milioni mbili na pia ameamuwa kuwa mlezi wa kikundi icho na amewataka kuamasishana kujiunga katika Vicoba na pia amewataka wale ambeo wanakopa mikopo wazilejishe kwa wakati ili na wegine nao wapate kuchukua mikopo, nawale watolo katika kikundi waache ili kukikuza kikundi maana utolo unazorotesha maendeleo.
Pia Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Kusin Unguja Mhe Mwantatu Mbarak Khamisi nae amesema kuwa mtaji wa milioni alubain si mdogo kwani kuna vikundi vingine vina kusanya na ikifikia kugawana basi mataji auonekani, amewashauri waongeze iodadi ya wanachama ambeo wanajishuulisha Katika Mkoa wa Kusini ili kikundi kiwi na wanachama wengi zaidi.
Pia Mwenyekiti wa Kikundi cha kikoba Ndg. Aziza Mnyimbi Makame asema lengo la kuanzisha kikundi ichi ni kujikwamua kiuchumi, kikundi icho walianzia kukopeshana lakimbili na mpaka sasa wanakopeshana mpaka milioni tatu na kilianzia na wanachama thelasini tu, wanamalengo ya kuwaongeza wanachama watakao taka kujiunga na kikundi chao kwani niayao ni kujikwamua kiuchumi asa zaidi kwa wakina mama wa Mkoa wa Kusini Unguja.
Lengo kuu la KIcoda ni kuweka na kukopa fedha ili kupunguza umasikini kwa kusomesha watoto wao, kilimo na Biashara. Kiwangocha kukopa kinaanzia shilingi 300,000 hadi 3,000,000 mkopo huo utegemea mahitaji ya mwanachama.
MATARAJIO ya kikundi icho ni kuhamasisha wanawake wengine wa Mkoa huo naopia kuunda vikundi kama wao na kuanzia Wilaya, jimbo wadi hadi Matawi ili kuongeza ufanisi wa vijana kujiongeza kufanya biashara mbalimbali.
Pia kina changamoto ya kikundi icho ni kuchelewa kwa ulejeshaji wa mikopo na hali ngumu ya uchumi baada ya kuingia na corona, utoro kwa baadhi ya wanachama.
Kikundu icho cha Vicoba ambacho kilianzishwa 31/12/2014 kina jumla ya wanachama 30 na niwanawake tu. Kina jumla ya shilingi milioni 40 na kina akiba yashilingi milion 32, jamii milioni 7,400,000 na adhabu kwa wanachama shilingi laki 6.
No comments:
Post a Comment