WAJASIRIAMALI FURSA NJE NJE KATIKA TAMASHA LA TATU LA ZANZIBAR KARIAKOO FESTIVAL.

Wajasiriamali wametakiwa kutumia fursa za matamasha kutanga biashara zao pia kuzingatia mafunzo wanayopatiwa katika kuboresha bidhaa zao

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa uwendeshaji na usafirishaji kutoka ofisi ya rais Fedha na mipango Ali Bakari Is- haka wakati akifungua tamasha la tatu la wajasiriamali la Zanzibar kariakoo festival kwaniaba ya Waziri wa nchi ofisi ya rais fedha na mipango Mh. Jamal Kasim huko katika viwanja vya kariakoo Mjini Zanzibar amesema.

ZSSF wamefanya kitu kizuri kwa kwa kuandaa maenesho hayo na kuwakutanisha wajasiriamali pamoja na kuwapa nafasi ya kujitangaza na kukuza biashara zao .

Aidha amewasisitiza wajasiria mali kujiunga na mfuko wa hiyari wa ZVSSF ili kunufaika na mafao yanayotolewa kama wanavyonufaika wafanyakazi wa wengine walioajiriwa.

Akizungumzia tamasha hilo Meneja wa kiwanja cha watoto Kariakoo Bw Hakim Foum amesema kuwa Tamasha Hilo ni Tamasha la tatu tokea kuaanzishwa ambapo Tamasha la Kwanza lilitwa kwa jina la Wasafi Festival ambalo Tamasha hilo  liliangalia masuala mazima ya burudani na katika Tamasha lapili liliangalia suala zima la nafasi ya Mwanamke katika sekta nzima ya  ujasiriamali.

Hata hivyo amesema katika tamasha hili la tatu kuna utofauti mkubwa kwani wajasiria mali wote watakuwa wakipatiwa elimu kuhusu ujasiriamali kutoka taasisi tofauti kwa siku zote kumi pia ameongeza kwakusema kuwa Zssf inaahidi kwa mwanachama yoyote wa mfuko wa hiyari ambae atachangi kwa miezi 9 basi tamasha lijalo atapata punguzo kwa asilimia hamsini.

Nae mkurugenzi muendeshaji wa ZSSF Bi Sabra Issa Machano amesema wajaria mali wanapata fursa ya kipekee ya kutangaza biashara zao pia kusajiliwa kwenye mfuko wa hiyari wa zvssf .

Pia ameongezea kusema kuwa kuongezeka kwa wadhamini kutoka taasisi mbalimbali za fedha ni ukuuwaji wa tamasha hilo.

Akizungumza kwaniaba ya wajasiriamali wenziwe ndugu Manju (Mama doux) amesema wanaishukuru ZSSF kwa kuwasamini na kuwatangaza kupitia tamasha hilo .

Tamasha la wajasiriamali la Zanzibar kariakoo festival limeandaliwa na mfuko wa hifadhi yajamii Zanzibar ZSSF ambalo ni la siku kumi limefunguliwa disemba 10 na linatarajiwa kukamilika Disemba 20, 2020



No comments:

Post a Comment