NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR DK. ABDULLAH JUMA SADALLAH AMPONGEZI RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHESHIMIWA DR. HUSSEIN ALI HASSAN MWINYI


Chama Cha Mapinduzi kinampongeza kwa dhati, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa kutimiza matakwa ya Katiba ya Zanzibar kwa kumchagua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Makamo wa Rais, Mheshimiwa Mazrui na Omar Said Shaaban kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.


Hakika Tukio hilo limedhihirisha nia ya dhati yake binafsi lakini pia ya Chama Cha Mapinduzi katika kutii matakwa ya Katiba kwenye uongozi wa nchi yetu.  Jambo hilo pia limethibitisha kauli zake za kuwa muumini wa Utawala Bora, Umoja wa Wazanzibari wenye kuthamini haki na wajibu wa Viongozi na wananchi wa Tanzania hususan Zanzibar.


Chama Cha Mapinduzi kinaunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais na Serikali yake hususan Mawaziri katika kuleta mageuzi ya utendaji kazi inaoitwa Management by walking around” yaani kutembea ni kuona na kuongoza kwa kushuhudia mwenyewe.  Chama kinaamini kuwa Viongozi waandamizi wengine watafata njia hii adhimu kuwa kama ndio Roda ya utendaji kazi katika ngazi zote.


Hakika tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuchagua Viongozi wepesi kujituma, kufatilia na kutoa maamuzi na wakati mwengine magumu yasiona muhali.  Napenda kuuhakikishia Umma kuwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Halmashauri za CCM katika ngazi ya Tawi, Wadi, Jimbo, Wilaya, Mkoa na Halmashauri Kuu ya Taifa.  Ngazi zote hizo kwa mpangilio maalum utaendelea kusimamia serikali kwa kila ngazi ili wananchi wafaidi matunda ya Mapinduzi chini ya Awamu hii ya nane inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi.



Chama Cha Mapinduzi pia kinamuahidi Rais wetu Mjumbe wa Kamati Kuu kuwa kitamuunga mkono katika harakati zake zote za mageuzi yeye binafsi na Viongozi Waandamizi wake wote.  Tunaamini Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi watashirikiana nae kwa kuleta mafanikio makubwa kwenye kuleta maendeleo ya Wazanzibari kiujumla.




  • - Kuundwa  kwa Taasisi ya Rais ya kufatilia Matokeo ya Maazimio “Presidential delivery Bureau” ni kielelezo cha wazi kuwa Serikali hatokaa mchana na usiku kufatilia Ilani ya Uchaguzi, ahadi za Mheshimiwa Rais, Wabunge na Wawakilishi tulipokuwa tunaomba ridhaa ya kuongoza Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
  • - Tunapinga vikali na tunaunga mkono juitihada za kubainisha fawahisha ubadhirifu wenye chembe chembe za ufisadi kila panapogundulika, Chama kinawaomba wanachama, wananchi, raia wema kuibua bila kusita masuala yoyote, yenye vituko vya uonevu, ubadhirifu, ufisadi na hata rushwa ya wazi au ya siri.


  • - Umoja wa Wazanzibari ndio nguzo pekee ya kudumisha amani na utulivu, na hivyo basi maendeleo ya kishindo tena ya muda mfupi.


  • - Chama Cha Mapinduzi kuwausia Wazanzibari wote walio ndani au nje ya nchi kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii lakini pia umoja, mshikamano na maendeleo ya kidugu miongoni mwa Wazanzibari wa rika, kabila, uzawa, dini na madhehebu yote.


  • - Chama Cha Mapinduzi kitasimamia sana maendeleo ya uchumi mdogo mdogo wa wananchi, wakulima, wavuvi, waendesha Bodaboda, mafundi mchundo na makundi tofauti (Micro Economic) ya watu wenye ulemavu, wanawake, wajane, yatima n.k. ili uchumi wa pamoja uwe na faida endelevu kwa faida ya wote.


  • - Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kutoa taarifa kila vikao na hadharani kwani tunaamini utendaji wa kazi kwa uwazi, jumuishi na shirikishi ndio njia muwafaka katika kuleta maendeleo ya haraka.

 

No comments:

Post a Comment