Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli amesema fomu za Maadili zisirudishwe kwa njia ya mtandao kwani mtu anayejua ‘passwords’ anaweza kuangalia fomu hizo na kujua siri za Mtu husika na kuharibu kwa kuwa wadukuzi wako wengi.
Akizungumza mara baada ya kumuapisha Kamishna wa Maadili, Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi amesema ni muhimu watu kuchukua fomu Mtandaoni lakini warudishe fomu hizo kwa kuzipeleka Tume ya Maadili na sio kuzituma njia ya Mtandao.
“Tulikubaliana kwamba fomu unazipakua, ukishajaza usizirudishe kwa mtandao, wanaojaza ni wengi ni vyema wazirudishe wenyewe mahali panapotakiwa, najua wasaidizi wako wamenielewa na inawezekana marehemu Jaji Nsekela ameshawapa maelekezo.”– Rais Magufuli
No comments:
Post a Comment