Akikabidhi vifaa hivyo Meneja Uendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa Jeremiah Mallongo katika Ofisi ya Wizara hiyo huko Mnazimmoja amesema wanatambua juhudi kubwa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupanga , kuratibu na kutekeleza mpango wa tahadhari katika kukabiliana na magonjwa hayo..
Amesema vifaa hivyo vitasaidia katika kupambana na kudhibiti maradhi ya kuambukiza ambayo yanarejesha nyuma soko na mfumo wa utalii na kudhorotesha biashara hiyo muhimu ya kukuza uchumi wa nchi.
Amesema vifaa hivyo vinathamani ya TZS millioni, 271,504,378 ambavyo vinajumuisha ICU Ventilators 4, Oxygen Concentrators 10, Respirators 2016, Examination Gloves 1000, Surgical Gowns 500 na Surgical Masks 4000 .
Aidha amesema shirika hilo litagharamia ufungaji wa vifaa tiba vyote katika sehemu ambazo wizara itaamua vifungwe mara baada ya uainishaji wa maeneo hayo utakapofanyika.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambae pia Mkurugenzi Tiba wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto Juma Salum Mbwana amesema wamepokea msaada wa vifaa hivyo na kuhakikisha watavitumia vizuri kwa lengo la kujikinga na magonjwa mbalimbali ili wananchi waishi katika hali ya salama na amani.
Aidha amesema vifaa hiyvo vitasaidia katika hali ya usalama kwa watalii watakao ingia nchini na kuwakumbusha kufuata taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha mikusanyiko inakuwa ya amani.
Baadhi ya Vifaa kinga vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wizara ya Afya
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Ustawi wa jamii Jinsia na Watoto Juma Salum Mbwana akitia saini hati ya makabidhiano msaada wa vifaa kinga mara baada ya makabidhiano huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar
Meneja Uwendeshaji Shirika la Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) Jeremiah Mallongo akitia saini hati ya makabidhiano msaada wa vifaa kinga mara baada ya makabidhiano huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar .
No comments:
Post a Comment