DK. MWINYI AONGOZA DUA MAALUM YA KUIOMBENCHI NA VIONGOZI WAKE AMANI KATIKA MSIKITI WA MUSHAWARRA MUEMBESHAURI UNGUJA ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhadj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Viongozi wa kisiasa wana dhima kubwambele Mwenyezi Mungu na kubainisha maridhiano ya kisiasa
yaliofanyika yameonyesha njia sahihi katika kudumisha umoja namshikamano nchini.

Alhadj Dk. Mwinyi amesema hayo katika Dua maalum ya kuiombeanchi na viongozi wake amani, hafla iliyofanyika katika Msikiti waMushawarra uliopo Muembeshauri Jijini hapa.Alisema kuna umuhimu kwa wananchi kumshukuru Mwenyezi Mungukwa kuwaongezea neema ya maridhiano yaliofanikisha uundaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.Alisema viongozi wana dhima kubwa ya kuhakikisha wanadumishaamani na mshikamano na hivyo akatumia fursa hiyo kumpongeza

Makamo wa Pili wa Rais, Maalim Seif Sharrif Hamad na Chama chake cha ACT Wazalendo kwa kukubali kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).Alisema yeye binafsi anaamini Wazanzibari wote ni kitu kimoja wakiwa na dhamira ya kuijenga Zanzibar na hivyo akawataka viongozi wa Dini kuendelea kuwaombea dua viongozi ili waendelee kuiongoza
nchi kwa ufanisi.

“Viongozi wana dhima kubwa kwa Mwenyezi Mungu …..maridhianoyaliofanyika yameonyesha mwelekeo sahihi wa nchi“Alieleza kuwa pamoja na Wazanzibari kuwa na mengi ya kumshukuruMwenyezi Mungu, pia wanapaswa kuendeleza amani iliopo nchini ili

kazi ya kuleta maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa iweze kufanikiwa. Alhadj Dk. Mwinyi alisema wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu uliopita alitowa ahadi nyingi sana kwa wananchi ikiwemo ile ya
kusisitiza kuendeleza amani na utulivu iliopo nchini pamoja na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kufanikisha azma hiyo.

Aidha, aliwataka Wazanzibari kufanya kazi kwa bidii kwa kila mmojakutekeleza wajibu wake kikamilifu mahala alipo ili kuleta ustawi wa maisha ya wananchi. Alitoa shukurani kwa wananchi wote wa Zanzibar kwa hatua zao za kumtumia pongezi kwa kuleta maridhiano na kubainisha kuwa hatua hiyo inaleta matumaini kuwa wananchi wengi wameridhia na kukubali
jambo hilo. 

Vile vile alisiitiza dhamira yake ya kuendelea kusimamia Umoja na mshikamano katika nchini ili kuharakisha kasi ya maendeleo.Alhadj Dk. Mwinyi alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea
kuibariki Zanzibar na kubaki katika hali ya mani, sambamba na kuwapongeza waandaaji wa Dua hiyo kwa kuona umuhimu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupokea maombi yao ,
ikizingatiwa dua kama hiyo ilifanyika kabla ya Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2020. 

Mapema, Waziri wa Nchi (OR) Katiba, sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman alitoa shukran kwa viongozi wakuu wa Kitaifa pamoja na wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo muhimu yenye faida kubwa kwa taifa.

Nae, Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Mfaume alisema dua hiyo inalenga kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na kumuombea Dua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhadj Dk. Hussein Ali Mwinyi na wasaidizi wake ili waweze
kutekeleza vyema majukumu yao ya kitaifa.

Viongozi mbali mbali wa kitaifa walihudhuria katika dua hiyo wakiwemo Marais Wastaafu Alhadj Amani Abeid Karume, Alhadj Ali Mohamed Shein, Alhadj Balozi Seif Ali Idd, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariamu Ali Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji, Mawaziri, Mwakilishi wa Mufti Mkuu kutoka Tanzania Bara heikh Alhad Mussa Salum pamoja na wananchi wa Mikoa ya Unguja.

No comments:

Post a Comment